KESHA LA ASUBUHI .
Alhamisi, 01/12/2022.
*YESU, MCHUNGAJI MKUU, ANAMJUA KILA KONDOO.*
*Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu. Luka 15:7.*
✍️ Mhudumu anapaswa kuwa mchungaji. Mkombozi wetu anaitwa Mchungaji mkuu. Mtume anaandika, "Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo." Hata tukiwa na hali ya chini kiasi gani, hata tuwe tumeinuliwa kiasi gani, kama tuko katika giza la shida au katika jua la mafanikio, sisi ni kondoo Wake, kundi la malisho Yake, na tuko chini ya uangalizi wa Mchungaji Mkuu.
✍️ Lakini Mchungaji mkuu anao wachungaji wake wadogo, ambao ameweka juu yao utunzaji wa kondoo na wana-kondoo Wake. Mchungaji mkuu kamwe hampotezi hata mmoja kutoka katika utunzaji Wake, kamwe haachi kumjali hata yule aliye dhaifu kabisa katika kundi Lake. Mfano mzuri ambao Kristo aliutoa wa kondoo mmoja aliyepotea, wa mchungaji aliyeacha tisini na tisa kwenda kumtafuta yule aliyepotea, unaeleza kwa mfano utunzaji wa Mchungaji mkuu. Hakuwaangalia kwa uzembe kondoo waliomo zizini, na kusema, "Ninao tisini na kenda, na itanigharimu taabu nyingi kwenda kumtafuta yule aliyepotea; hebu na arudi, nami nitamfungulia mlango wa zizi la kondoo na kumruhusu aingie; lakini siwezi kwenda kumtafuta."
✍️ Hapana; kwa maana mara tu kondoo yule anapopotea uso wa mchungaji hujawa na huzuni na wasiwasi. Anahesabu na kuhesabu tena kundi, na pale anapokuwa na hakika kwamba kondoo mmoja amepotea, hasinzii. Anawaacha wale tisini na tisa ndani ya zizi; haidhuru usiku ni wenye giza na dhoruba kiasi gani, haidhuru njia ni ya hatari na mbaya kiasi gani, haidhuru utafutaji ni wa muda mrefu na mgumu kiasi gani, yeye hachoki, hasiti, hadi yule aliyepotea amepatikana.
✍️ Lakini anapopatikana, je, anatenda bila kujali? Je, anamwita kondoo yule na kumwamrisha aliyepotea kumfuata? Je, anamtishia na kumpiga, au kumswaga mbele yake, akisimulia uchungu na mfadhaiko na wasiwasi ambao amepata kwa ajili yake? Hapana; yeye humlaza juu ya bega lake kondoo yule aliyetanga-tanga aliyechoka, aliyeishiwa nguvu, na kwa shukrani ya uchangamfu kwamba utafutaji wake haujawa bure, anamrudishia zizini. Shukrani yake hudhihirishwa na nyimbo tamu za furaha, na kwaya za mbinguni huitikia noti ya furaha ya mchungaji.
✍️ *Aliyepotea anapopatikana, mbingu na nchi huungana katika kushangilia na kushukuru.... Yesu anasema, "Mimi ndimi mchungaji mwema, nao walio wangu nawajua, nao walio wangu wanijua mimi." Kama vile wachungaji wa dunia wanavyowajua kondoo zao, ndivyo Mchungaji Mkuu anavyolijua kundi Lake ambalo limetawanyika kote ulimwenguni.-The Review and Herald, Agosti 23, 1892.*
*MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA.*
🙏🙏🙏🙏
YESU, MCHUNGAJI MKUU, ANAMJUA KILA KONDOO
Reviewed by Inspirit Academy
on
noviembre 30, 2022
Rating:
No hay comentarios: