WATU WALIOONGOKA KWELI HULENGA KUFIKIA UKAMILIFU

KESHA LA ASUBUHI 

JUMAMOSI, DESEMBA 03/12/2022

WATU WALIOONGOKA KWELI HULENGA KUFIKIA UKAMILIFU

Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. Mathayo 5:48.
▶️ Kuna maana kubwa sana kuwa Mkristo thabiti. Kunamaanisha kutembea kwa uangalifu mbele za Mungu, kusonga mbele kuelekea alama ya tuzo ya mwito wetu mkuu katika Kristo. Kunamaanisha kuzaa matunda mengi kwa utukufu wake Yeye aliyemtoa Mwanawe afe kwa ajili yetu. Kama wana na binti za Mungu, Wakristo wanapaswa kujitahidi kufikia ubora wa juu uliowekwa mbele yao katika injili. Hawapaswi kuridhika na kitu kingine chochote pungufu ya ukamilifu....
▶️ Hebu tulifanye Neno takatifu la Mungu kuwa somo letu, tukileta kanuni zake takatifu maishani mwetu. Hebu tuenende mbele za Mungu kwa upole na unyenyekevu, tukisahihisha makosa yetu kila siku. Hebu kwa kiburi cha ubinafsi tusiitenganishe roho na Mungu. Usilee hisia ya fahari ya juu kabisa, ukijifikiria mwenyewe kuwa bora kuliko wengine. "Anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke." Amani na pumziko vitakuja kwako pale utakapoyaleta mapenzi yako kuwa chini ya mapenzi ya Kristo. Ndipo upendo wa Kristo utatawala moyoni, ukiteka nyara kwa Mwokozi chemchemi za siri za utendaji. Hasira ya haraka, inayoamshwa kwa urahisi itatulizwa na kutiishwa na mafuta ya neema ya Kristo. Hisi ya dhambi zilizosamehewa italeta amani ile ipitayo ufahamu wote. Kutakuwapo na jitihada ya dhati ya kuyashinda yote yanayopingana na ukamilifu wa Kikristo. Tofauti itatoweka. Watu ambao wakati fulani waliwakosoa wale walio karibu nao wataona kwamba makosa makubwa zaidi yapo katika tabia zao wenyewe.
▶️ Kuna wale wanaousikia ukweli, na kusadikishwa kwamba wamekuwa wakiishi kinyume na Kristo. Wanahukumiwa, na kutubu dhambi zao. Wakizitegemea stahili za Kristo, wakitumia imani ya kweli Kwake, wanapokea msamaha wa dhambi. Kadiri wanapoacha kufanya maovu na kujifunza kufanya mema, wanakua katika neema na katika kumjua Mungu. Wanaona kwamba ni lazima watoe kafara ili kujitenga na ulimwengu; na baada ya kuhesabu gharama, wanaangalia yote kama hasara ikiwa tu wataweza kumpata Kristo. Wamejiandikisha katika jeshi la Kristo. Vita viko mbele yao, na wanaviingia kwa ujasiri na uchangamfu, wakipigana vita dhidi ya mielekeo yao ya asili na tamaa za ubinafsi, wakileta mapenzi yao chini ya mapenzi ya Kristo. Kila siku wanamtafuta Bwana kwa ajili ya neema ya kuwawezesha kumtii, nao wanaimarishwa na kusaidiwa.
🔘 Huu ni uongofu wa kweli. Kwa utegemezi wa unyenyekevu, wa shukrani wale ambao wamepewa moyo mpya wanategemea msaada wa Kristo. Wanadhihirisha katika maisha yao tunda la haki. Awali walijipenda wenyewe. Anasa za dunia ndizo zilikuwa furaha yao. Sasa kipenzi chao kimeondolewa katika kiti cha enzi, na Mungu ndiye mtawala mkuu.-Youth's Instructor, Sept. 26, 1901


MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA
WATU WALIOONGOKA KWELI HULENGA KUFIKIA UKAMILIFU WATU WALIOONGOKA KWELI HULENGA KUFIKIA UKAMILIFU Reviewed by Inspirit Academy on diciembre 02, 2022 Rating: 5

No hay comentarios:

Con la tecnología de Blogger.