KESHA LA ASUBUHI
JUMAMOSI, NOVEMBA 26/11/2022
TUNAPASWA KUKUA KATIKA UCHAJI MUNGU, USAFI NA UPENDO
Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili. 1 Petro 2: 2, 3.
✍️ Mungu amefanya kila majaliwa kwa ajili ya kuokoa kila roho; lakini tukiikataa kwa dharau karama ya uzima wa milele, iliyonunuliwa kwa ajili yetu kwa gharama isiyo na kikomo, wakati utakuja ambapo Mungu pia atatusukumia mbali kutoka katika uwapo wake, kama sisi ni matajiri au maskini, sisi ni wakuu au wa chini, wenye elimu au wasio na elimu. Kanuni za haki ya milele zitakuwa na utawala kamili katika siku ile kuu ya ghadhabu ya Mungu.
✍️ Hatutasikia shitaka dhidi yetu katika msingi wa dhambi za mlipuko tulizotenda, bali shitaka litafanywa dhidi yetu kwa sababu ya kupuuza wajibu mzuri na wa kiadilifu ulioamriwa kwetu na Mungu wa upendo. Mapungufu ya tabia zetu yataoneshwa wazi. Hapo ndipo itakapojulikana kwamba wote waliohukumiwa kwa jinsi hiyo walikuwa na nuru na maarifa, walikabidhiwa mali za Bwana wao, nao wakaonekana kutokuwa waaminifu kwa dhamana yao. Itaonekana kwamba hawakufurahia dhamana ile ya mbinguni, kwamba hawakutumia mtaji wao katika utumishi wa upendo kwa wengine, kwamba kwa kanuni na fano hawakukuza imani na upendo kwa wale walioshirikiana nao. Itakuwa ni kulingana na nuru ambayo wamekuwa nayo watahukumiwa na kuadhibiwa.
✍️ Mungu anataka kwamba kila wakala mwanadamu atumie vizuri njia zote za neema ambazo mbingu imetoa, na kuwa na ufanisi zaidi na zaidi katika kazi ya Mungu. Kila mpango umefanywa ili kwamba uchaji Mungu, usafi, na upendo wa wafuasi wa Kristo uzidi kuongezeka daima, ili vipaji vyao vipate kuongezeka maradufu, na uwezo wao uongezeke katika utumishi wa Bwana wao wa kiungu.
🔘 Lakini ingawa mpango huu umefanywa, wengi wanaokiri kumwamini Yesu hawaufanyi udhihirike kwa ukuaji ule unaoshuhudia nguvu ya kutakasa ya ukweli juu ya maisha na tabia. Tunapompokea Yesu kwa mara ya kwanza mioyoni mwetu, tunakuwa kama watoto wachanga katika dini; lakini hatupaswi kubakia kuwa watoto wachanga katika uzoefu. Tunapaswa kukua katika neema na katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo; tunapaswa kufikia kipimo kamili cha kimo cha wanaume na wanawake ndani yake. Tunapaswa kufanya maendeleo, kupata uzoefu mpya na mwingi kupitia imani, tukikua katika tumaini na imani na upendo, tukimjua Mungu na Yesu Kristo aliyemtuma. -Youth’s Instructor, June 18, 1893
MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA
TUNAPASWA KUKUA KATIKA UCHAJI MUNGU, USAFI NA UPENDO
Reviewed by Inspirit Academy
on
noviembre 25, 2022
Rating:
No hay comentarios: