KESHA LA ASUBUHI
JUMANNE, NOVEMBA 29 2022
TUNAPOONA KIU YA HAKI, YESU ANASOGEA KARIBU
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu, Mungu aliye hai. Zaburi 42:1, 2.
Bwana ana kweli za maana sana za kuwafunulia wale ambao wangeweza kuelewa mambo ya Roho. Masomo yake ni kwa ajili ya wote, nayo yametengenezwa yapate kufaa kwa mahitaji ya wote. Ingawa masomo Yake yamevikwa kwa lugha rahisi ili mtoto apate kuyaelewa, ukweli ni wa kina kiasi kwamba msomi kabisa anaweza kuvutiwa hasa, na kumwabudu Mwanzilishi wa hekima isiyo na kifani. Ingawa mwenye hekima kabisa anaweza kupata mambo tele ya kuwazia katika usemi Wake sahili kabisa, wanyenyekevu kabisa wanaweza kuelewa ukweli Wake, na kutumia ahadi Zake kwa hitaji la roho.
Yesu aliwafundisha wanaume na wanawake kwa kusudi la kuamsha shauku ya kuelewa mambo ya Mungu, ili waweze kuona ubora wa tabia ya kiungu, na kutumia haki ya Kristo, ambayo ndani yake wangeweza kusimama wakikubaliwa mbele za Bwana Yehova.
Je! una hisi ya upungufu katika roho yako? Je, una njaa na kiu ya haki? Basi huu ni ushahidi kwamba Kristo ametenda kazi moyoni mwako, na kuiumba hisi hii ya uhitaji ndani ya roho yako, ili apate kutafutwa akutendee, kwa majaliwa ya Roho Mtakatifu, mambo yale ambayo haiwezekani wewe kujitendea mwenyewe....
Mifano ya Kristo imewekwa katika kumbukumbu, na kwa mchunguzaji mwaminifu wa ukweli, mwenye bidii, maana yake itawekwa wazi, siri zake zitafunuliwa. Wale ambao hawatautafuta ukweli kama hazina iliyositirika wanadhihirisha ukweli kwamba kwa kweli hawataki kujua ukweli ni nini. Kristo bado anawaambia wafuasi wake wa kweli, "Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni." "Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele."
Wale wanaoitikia ushawishi wa Kristo wataonekana wakiuliza kuhusu ukweli ni nini, ili miguu yao ipate kuelekezwa katika njia ya haki. Kristo anawavuta wote, lakini si wote wanaitikia ushawishi wake. Wale ambao wanayaacha mapenzi yao kwa sababu ya mapenzi ya Mungu, ambao wako tayari kufuata kokote ambako Roho wa Mungu anaweza kuongoza, ambao wanapokea nuru na kutembea ndani yake, bado watatafuta elimu zaidi ya mbinguni, na "atazidishiwa tele."-The Signs of the Times, Novemba 7, 1892.
MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA
TUNAPOONA KIU YA HAKI, YESU ANASOGEA KARIBU
Reviewed by Inspirit Academy
on
noviembre 28, 2022
Rating:
No hay comentarios: