UWE MUUNGANA, KUWAFARIJI WENGINE, KAMA ALIVYOFANYA YESU

KESHA LA ASUBUHI 

IJUMAA, NOVEMBA 25/11/2022

UWE MUUNGANA, KUWAFARIJI WENGINE, KAMA ALIVYOFANYA YESU

Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka. 1 Petro 3:8, 9.
⏯️ Wale wanaofanya kazi kwa ajili ya Kristo wanapaswa kuwa wasafi, wanyofu, na wa kutegemewa, na pia wanapaswa kuwa wapole, wenye huruma na waungwana. Kuna mvuto katika kushughulikiana na katika mazungumzo ya wale ambao ni waungwana wa kweli. Maneno mazuri, mionekano ya kupendeza, mwenendo wa kiungwana, ni vya thamani isiyokadirika. Wakristo wasio waungwana, kwa kuwapuuza wengine, wanaonesha kwamba hawako katika umoja na Kristo. Haiwezekani kuwa katika umoja na Kristo na bado usiwe muungwana.
⏯️ Kile ambacho Kristo alikuwa katika maisha yake hapa duniani, kila Mkristo anapaswa kuwa. Yeye ni mfano wetu, si tu katika usafi wake usio na doa lakini pia katika uvumilivu wake, upole, na kupendeza kwa tabia. Alikuwa thabiti kama mwamba pale ambapo ukweli na wajibu vilihusika, lakini kila wakati alikuwa ni mkarimu na mwenye adabu. Maisha yake yalikuwa kielelezo kamili cha uungwana wa kweli. Daima alikuwa na mwonekano wa wema na neno la faraja kwa wahitaji na walioonewa.
⏯️ Uwapo Wake ulileta mazingira safi zaidi nyumbani, na maisha Yake yalikuwa kama chachu ifanyayo kazi katikati ya misingi ya jamii. Asiye na madhara na asiye na unajisi, Alitembea miongoni mwa wasiowafikiria wenzao, mafidhuli, wasio na adabu; miongoni mwa watoza ushuru wadhalimu, Wasamaria waovu, askari wapagani, wakulima wakali, na umati wa watu waliochanganyika. Alizungumza neno la huruma hapa, na pale, alipowaona watu waliochoka, na kulazimika kubeba mizigo mizito. Alishiriki mizigo yao, na akayarudia kwao masomo yale aliyokuwa amejifunza kutoka katika asili yale upendo, huruma, wema wa Mungu.
⏯️ Alitafuta kuwatia moyo kwa kuwapa tumaini wale waliokuwa wakali na wasioelekea kutenda mema, akiweka mbele yao uhakikisho kwamba wangeweza kuwa watu wasio na hatia na wapole, wakifikia tabia ile ambayo ingewafanya kujidhihirisha kama watoto wa Mungu....
🔘 Upendo wa Kristo huchangamsha moyo na kulainisha ukali wote kutoka katika tabia. Hebu tujifunze kutoka Kwake jinsi ya kuchanganya hisi ya juu ya usafi na uadilifu na uchangamfu wa tabia. Mkristo mwema, muungwana ndiye hoja yenye nguvu kabisa inayoweza kutolewa katika kuunga mkono injili. -The Review and Herald, Agosti 20, 1959.



MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA
UWE MUUNGANA, KUWAFARIJI WENGINE, KAMA ALIVYOFANYA YESU UWE MUUNGANA, KUWAFARIJI WENGINE, KAMA ALIVYOFANYA YESU Reviewed by Inspirit Academy on noviembre 24, 2022 Rating: 5

No hay comentarios:

Con la tecnología de Blogger.