Mateso hulisafisha kanisa

 

MATESO HULISAFISHA KANISA.


Mafanikio huzidisha watu wengi wanaodai kuamini. Ila pindi mateso ya kuifia dini na kuwa mwaminifu mpaka kufa kwa ajili ya kuitetea imani wengi wataikana imani na kuiacha.


Wakati haupo mbali sana ambapo kila mtu atatahiniwa.

Chapa ya mnyama itashurutishwa kwetu, na wale ambao wamejisalimisha hatua kwa hatua katika matakwa ya ulimwengu na kufuatisha katika desturi za kidunia hawataona kuwa ni jambo gumu kwao kujisalimisha chini ya mamlaka ya mpinga Kristo.

Watu wengi watahofia kufilisiwa mali, kufukuzwa kazi, kufungwa, au kutukanwa na kunenewa majina mabaya kama wafarakanisha na wachochezi.

Wengi watajitenga na imani kwa kuhofia kupoteza maisha yao ya kimwili.

Wakati haupo mbali ambapo kila mmoja ataitetea imani yake kwa damu yakemwenyewe.

Tunaishi katika kipindi mhimu sana cha utimiaji wa unabii, kila kitu kilichotabili kinatimia upesi sana.

Kila mmoja anawajibu wa kutambua majira tuliyonayo na kuishi kufuatana na mapenzi ya aliye juu.

Maandiko yanasema kutakuwa na wakati mgumu ambao tokea kuumbwa kwa ulimwengu haujawahi kuwepo.

Na kama siku hizo za mateso sizingelifupishwa hakuna hata mmoja angeokoka.

Dunia kwa sasa imejaa vilio kila mahari, ugaidi, njaa, tauni, magonjwa, vita, na mengine mengi yamewafanya watu kulia usiku na mchana wakihitaji msaada wa

hari na mali.

Ndugu zangu niwaambie tu kuwa mambo haya maovu yanayotendeka chini ya mbingu hayataisha wala kukoma mpaka Kristo atakaporudi mara ya pili.

Kwa hiyo kila mmoja anawajibu wa kujitakasa na kukaa karibu zaidi na Mungu kuliko wakati mwingine, maana maandiko yanasema heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa.

Mateso hulisafisha kanisa Mateso hulisafisha kanisa Reviewed by Inspirit Academy on septiembre 30, 2021 Rating: 5

No hay comentarios:

Con la tecnología de Blogger.